Kosa la kiusalama katika iPhone 6s lagunduliwa

Jose Rodriguez kwa mara nyingine amegundua mwanya katika mfumo wa baadhi ya simu za iPhone 6s ambao unaweza kumpa mtu nafasi ya kuona mawasiliano na picha katika simu ya iPhone ambayo imefungwa na lock.
Hii sio mara ya kwanza kwa jamaa huyu kugundua tatizo kama hili katika iPhone kwa sababu mwaka jana pia aligundua tatizo kama hilo, lakini pia hii siyo mara ya kwanza kwa Apple kufanya kosa kama hilo ambalo linawaweka watumiaji wa vifaa vyao katika hatari ya uhalifu wa kimtandao.
Mwanya ambao umegunduliwa katika simu za iPhone 6s unaruhusu mtumiaji bila ya kuwa na password ama nywila sahihi kuweza kuona mawasiliano ama contacts, ama picha ambazo zipo katika simu hizo. Kwa kutumia msaidizi wa simu hizo Siri ambaye anauwezo wakufanya kazi kwa kutumia amri ya sauti hata wakati simu ikiwa imefungwa, Siri akijaribu kumsaidia mtumiaji anajikuta anatengeneza mwanya wa mtumiaji asiye na password kuweza kuona taarifa ambazo ki msingi zilitakiwa ziwe zimefungwa.
Utumiaji wa huduma ya Siri ilikuwa inamuwezesha mtu kuweza kutumia mambo mengi bila ya ku’unlock simu
Siri inapotumika kutafuta taarifa fulani katika Twitter kwamfano na ikatokea kwamba moja ya matokeo yake yanahusisha majibu ambayo yanaweza kuhifadhiwa kama vile barua pepe basi katika kuhifadhi huku kumbukumbu hiyo itakuwa ni rahisi kuona kumbukumbu nyingine ambazo zipo katika simu hiyo na pia kama utataka kuunganisha anuani hiyo pamoja na picha basi utaweza kuchagua picha ambazo zipo katika kumbukumbu ya simu hiyo na hivyo kukupa nafasi ya kuziona picha zilizo ndani ya simu iliyofungwa.
Hata hivyo sio kila simu ya iPhone 6s ina mwanya huu, ni zile tu ambazo zimefanyiwa mpangilio ambao unaruhusu Siri kuitumia Twitter katika kutafuta vitu. Kwa maana hiyo ili kuepuka dhahama hii watumiaji wa iphone 6s wanatakiwa kuhakikisha kwamba wameondoa mpangilio ambao unampa siri ruhusa ya kupekua mpaka katika Twitter pindi anaapoambiwa atafute kitu.
Tatizo hili limetatuliwa na Apple katika toleo jipya la iOS 9.3.1 update ambayo imekwisha anza kupatikana.
Teknokona inawashauri wote ambao wanatumia hizi simu kufanya utaratibu wa kuweza kuzuia uwezekano wowote wa taarifa zao kudukuliwa kwa kushusha na kuinstall update ya iOS

Previous
Next Post »

Ads Inside Post