Groups za WhatsApp kusajiliwa huko India, Maadmin hatiani Kufungwa

Serikali ya wilaya moja nchini India, Kupwara, imetambulisha utaratibu mgumu kweli kweli kwa watumiaji wa WhatsApp katika eneo lao. Utaratibu huo utawabana ma’admin wa groups pale kosa linapotendwa katika makundi waliyoyaanzisha.
Pia wafanyakazi wa serikali wameambiwa wasijihusishe na ma’group ya habari na kwamba mfanyakazi wa serikali akigundulika anashiriki katika kuongelea sera za serikali katika magroup ya WhatsApp basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Makundi yote ya WhatsApp yanatakiwa kuhakikisha yamejiandikisha kwa mkuu wa wilaya hiyo. Na moja ya hatua inayochukuliwa katika uandikishaji huo inaonekana ni kuingiza namba ya chombo cha usalama katika magroup hayo ili kurahisisha ufuatiliaji wa mazungumzo.
Je una maoni gani juu hili? Ni jambo zuri au baya? Tayari watu wengi wanalipinga wakisema uongozi wa eneo la Kupwara huko India umepitiliza mipaka.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post