Apple wametambulisha simu yao mpya ya iPhone SE, ambayo imepata sifa ya kuitwa simu ya bei nafuu zaidi kuwahi kutolewa na Apple. Nafuu???? Si wote watakubali…

Apple wametambulisha simu yao mpya ya iPhone SE, ambayo imepata sifa ya kuitwa simu ya bei nafuu zaidi kuwahi kutolewa na Apple. Nafuu???? Si wote watakubali…
Katika utambulisho wa simu hiyo uliofanyika jana nchini Marekani toleo la simu ya iPhone SE linalenga kuzidi kuongeza mauzo ya simu za iPhone katika masoko ya nchi zinazoendelea na ata zile zilizoendelea ambazo watumiaji flani wanaona matoleo kama iPhone 6S na iPhone 6S Plus ni ghali sana.
Pia inasemekana uamuzi wa iPhone kuanza nao kutoa simu zenye maumbo makubwa kama vile kwa Samsung kuliwaaudhi baadhi ya wateja wao wasiopenda simu zenye maumbo makubwa.
Bei?
Simu ya iPhone SE itaanza kupatikana kwa dola 399 za marekani (Tsh 875,000/= | Kes 40,500/= ) kwa toleo la GB 16 na huku la GB 64 litapatikana kwa dola 499.
Sifa za iPhone SE
Ina teknolojia za 2G, 3G na LTE – WiFi
Chipi ya A9 – 64Bit
Ukubwa wa inchi 4
Kamera ya Megapixel 12 (f/2.2, 29mm, autofocus, dual-LED (dual tone) flash)
Inasemekana ndani yake ina RAM ya GB 2
Kwa kifupi iPhone SE ni simu janja yenye umbo dogo ila yenye uwezo mkubwa sana. Suala la bei bado wengi wanaona ingawa ni bei ya chini ukilinganisha na matoleo mengine ila bado ipo juu – ‘ila ndio hivyo tena, kitu tayari kinaitwa iPhone’, lazima bei iwe ghaghariiii a.k.a Ndi Ndi Ndi
iPhone SE kushoto zikiwa pamoja na iPhone 6S, 6S Plus, 6 na 6 Plus
Inasemekana watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, India n.k waliokuwa wanatamani kumiliki simu mpya kabisa ya iPhone wataweza kufanya hilo kwa mara ya kwanza. Kwani ingawa ina umbo dogo, bado ni simu inayovutia na inayopatikana kwenye bei iliyo chini ukilinganisha na matoleo mengine.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post