Mkuu wa shule ya sekondari Buswelu jijini Mwanza pamoja na makamu wake wanashikiliwa na polisi kwa maagizo ya mkuu wa mkoa wa Mwanza baada ya kukutwa na mihuri 29 ya taasisi mbalimbali za shule kinyume cha sheria.
Kufuatia hatua hiyo mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo amemwagiza katibu tawala wa mkoa huo kumvua cheo cha ukuu wa shule huku sheria dhidi ya tuhuma zinazomkbali mkuu huyo zikifuata mkondo wake.
Mwalimu huyo aliyejulika kwa jina la Deogratias Lwakapamba mkuu wa shule ya sekondari Busweru alikamatwa na mihuti 29 ya taasisi mbalimbali za shule kinyume cha sheria .
Imearifiwa kuwa shughuli ya mihuri hiyo ilikuwa ni kutengeneza uhamisho bandia, fomu feki za TSM9 pamoja na kughushi uhamisho kutoka shule za binafsi huku akijipatia fedha kwa wale waliokosa sifa ya kuendelea na masomo ya sekondari katika shule nyingine
Tuhuma nyingine alizokutwa nazo mwalimu huyo ni pamoja na kuiba mali za shule, kuwadhalilisha walimu wenzake na kuchangisha michango kadha ili hali serikali ilipiga marufuku hatua hiyo.
Licha ya makamu wake mwalimu Manishe Ngeze kudai kuwa hajawai kushirikishwa katika tuhuma za ubadhilifu zinazo mkabili mkuu wake lakini hakuweza kusamehema katika tuhuma hizo
Hii ni taswira nyingine katika sekta ya elimu jijini Mwanza ikiwa ni juzi tu walimu watono kati ya nane wa shule ya sekondari Mihama wameswekwa rumande kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi wao.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon