Leawo Music Recorder: Rekodi muziki na sauti kwenye Kompyuta kwa Urahisi!

Unasikiliza nyimbo au kitu flani kutoka kwenye mtandao na unataka urekodi ili uweze sikiliza baadae? Au ata sauti kutoka kwenye muvi n.k…programu ya Leawo Music Recorder ni programu inayoweza fanya hayo yote.
Kupitia programu ya Leawo Music Recorder utaweza;
Kurekodi nyimbo au sauti yeyote inayocheza kutokea kwenye programu nyingine au kwenye mitandao kama vile YouTube n.k
Kurekodi sauti kutoka kwenye kinasa sauti (Mic) ulichounganisha na kompyuta yako
Pia unaweza kwa kutumia Task Scheduler kuipangia muda wa kuanza na kuacha kurekodi ata pale ambapo aupo (Kujua kuhusu Task Scheduler soma -> Jinsi ya Kuiwezesha Kompyuta Kujizima Yenyewe Usiku
Pale utakaporekodi wimbo unaotumbulika programu hii itakusaidia kukuwekea picha ya albam, na taarifa zingine muhimu kama vile jina la wimbo n.k. (itaitaji uwe na intaneti)
Pia utaweza kufanya marekebisho (edit) ya mafaili ya muziki uliyoyarekodi
Mafaili ya nyimbo ulizorekodi unaweza zitumia/sikiliza kwenye programu nyingine yeyote kwani yatakuwa kwenye mfumo uupendao wewe, mfano, mp3.
Mfano; Nimecheze wimbo wa Eminem wa Toy Soldiers kwenye Spotify kisha nikafungua Leawo na kurekodi. Kwa kuwa nina intaneti programu hiyo ilichukua moja kwa moja taarifa za wimbo huo na kuziweka kwenye faili hili jipya la mp3 lialotengenezwa kupitia kurekodi
Programu hii inatengenezwa na kupatikana kupitia mtandao wa Leawo. Wanaprogramu nyingine mbalimbali ukiacha Leawo Music Recorder, karibia zote utaweza tumia bure kwa siku kadhaa tuu baada utatakiwa kulipia.
Kwa muda mchache ambao nimekuwa natumia naweza kusema na programu nzuri inayoweza wasaidia watu wanaopenda kusikiliza miziki mitandaoni n.k. Changamoto yake ni bei yake tuu, leseni ya programu hii baada ya muda wa bure kutumia ni dola 19.99 za kimarekani. Kwa watu wenye matumizi ya kawaida wanaweza ona ni bora kutafuta njia zingine.
Je unafahamu programu nyingine unayoitumia kufanikisha hayo tuliyoyataja? Tuambie kupitia kwenye comment.
Kwa watumiaji wa Mac, Windows XP, Vista, 7, 8, 8.1, na 10… Unaweza kushusha na kupakua programu hii kutoka hapa -> Leawo Music Recorder
[Tunawashukuru LEAWO.COM kwa kuwezesha upatikanaji wa Activation code hizi]

Previous
Next Post »

Ads Inside Post