TrueCaller bado inakuwa ndio chanzo bora cha kumgundua muwasilianaji kwa kutoa jina au namba ya simu kwa kipindi cha muda wa miaka 6 mpaka sasa.
TrueCaller ni App nzuri sana ya kukuonyesha jina halisi la muwasilianaji wako na pia App hii inapatikana karibia katika kila soko la App za simu kama vile Google Playstore ya Android na AppStore ya iOs.
Japokuwa App ina sifa nyingi kuliko ubaya lakini inawezekana kuwa ukawa hupendi watu kuona au kujua namba yako pindi wanapotumia App hii basi hapo unaweza ukaiondoa kwa urahisi tuu.
TrueCaller inakupa hayo mamlaka (ya kuweza kuondoa) na leo TeknoKona itaenda na wewe sambamba kuhakikisha unaweza fanya hivyo.
JINSI
TrueCaller inakupa mamlaka yote ya kuweza kufuta namba yako katika hifadhi yake, unaweza fanya hivyo kiurahisha kwa kujitoa katika huduma hii kwa kutumia njia ifuatayo
Kwanza kabisa itakubidi u ‘deactivate’ (uipumzishe kwa muda) akaunti yako ya TrueCaller
Jinsi Ya Ku ‘Deactivate’
Fungua App ya TrueCaller katika simu janja yako
Nenda katika Eneo la ‘settings’ na kisha chagua ‘About TrueCaller’
Ukiwepo hapo chagua ‘Deactivate Account’ na kisha bofya ‘Yes’
Ukifanya hivyo utakuwa umepumzisha akaunti yako ya TrueCaller kwa muda na unaweza ukaendelea katika kuifuta namba yako kabisa katika hifadhi ya TrueCaller …. Ngoja tuone njia
Bofya link hii baada ya kuipumzisha akaunti yako ya Truecaller kwa muda
Sehemu Ya ‘UnList’ Katika TrueCaller
Weka namba yako ya simu ikianziwa na namba ya utambulisho wanchi
Ingiza maneno/namba utakazoziona kwa lengo la kujua utambulisho
Sasa unaweza ukabofya ‘Unlist’ (yaani kujitoa kabisa)
Safi sasa namba yako itatolewa katika kumbukumbu za TrueCaller ndani ya masaa 24 na pia hakuna mtu yeyote ambae ataweza kukupata kwa kutumia TrueCaller na pia hata wewe hutaweza kutumia TrueCaller ili kugundua watu mbalimbali – mpaka ujiunge tena – Ni matumaini yabgu kuwa umeweza kufuta na kuiondoa namba yako katika hifadhi ya TrueCaller
Kama unapitia tatizo lolote katika kufanya hivyo tuandikie sehemu ya comment hapo chini na sisi tutarudi tena kwako. Pia niambie kama njia hii imekusaidia. Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari moto moto za kiteknolojia. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon