Waethiopia 83 walioingia nchini bila vibali wahukumiwa miaka mitatu jela na mahakama ya Iringa.

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa
imewahukumu kwenda jela miaka mitatu
wahamiaji 83 raia wa Ethiopia walioingia nchini
bila kibali huku pia ikiwahukumu jela miaka
mitano dereva na utingo wa lori waliowasafirisha
wahamiaji hao kutoka jijini Dar es Salaam
kuelekea nchini Malawi.
Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo hakimu
mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa
wa Iringa Mheshimiwa Edrew Scout amesema
mahakama imezingatia maombi yote ya wahusika
lakini kwakuwa biashara ya usafirishaji binaadam
imezidi kushamili nchini mahakama imeona ni
vema watuhumiwa hao wakatumikia adhabu ya
kufungwa jela miaka mitatu au faini ya shilingi
milioni moja na kurejeshwa kwao baada ya
adhabu.
Mahakama hiyo imewakuta na hatia dereva na
utingo wa lori lililowasafirisha wahamiaji hao
Hance Mwakyoma na Alex Adam kwenda jela
miaka mitano au faini ya shilingi milioni moja na
nusu ambapo dereva wa lori Bwana Hance
Mwakyoma amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Katika kesi nyingine ya wahamiaji 12 raia wa
Ethiopia waliokamatwa hivi karibuni wakiwa
kwenye gari ya kusafirisha magazeti ya kampuni
hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu makazi
ya mkoa wa Iringa Richard Kasele
amewahukumu kwenda jela miaka miwili au
kulipa faini ya shilingi laki tano watuhumiwa hao
huku kesi ya dereva wa gari lililowasafirisha
pamoja na wasaidizi wake wawili ikiahirishwa
hadi tarehe 15 mwezi huu.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post