TFF yampongeza Kikwete kwa kuteuliwa na CAF

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia
(TFF), Jamal Malinzi amempongeza Rais wa
awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kukubali
uteuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani
Afrika (CAF) na GAVI utakaomfanya kuwa bingwa
wa chanjo na balozi wa mradi wa Africa United
Duniani.
“Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa
chanjo na hasa katika maendeleo ya vipaji na
wanamichezo kwa ujumla na jinisi chanjo
inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya
maendeleo bali pia haki ya kuishi” ilisema
sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa
TFF, Jamal Malinzi.
Katika barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya
TFF kuona kiongozi wa Tanzania akiongoza
mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi
cha sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa
ujumla.
“TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha
malengo yaliyowekwa na ushirika wa chanjo”
ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake
imetumwa kwa Rais wa CAF

Previous
Next Post »

Ads Inside Post