Huwezi ukataja mageuzi kumi ya teknolojia
mwaka huu bila ya kutaja Chaja za wireless,
ukweli ni kwamba haya ndiyo mageuzi ya
pekee ambayo yamegusa watengenezaji wengi
tofauti tofauti wa vifaa pia teknolojia hii
imegusa aina nyingi za vifaa kutoka saa janja
simu janja hadi vifaa vya viwandani kama
magari.
Mafanikio ya teknolojia hii ya chaja za
wireless inakuja kutokana na ukweli kwamba ni
rahisi mno kuitumia, ni rahisi kuweka simu
yako juu ya chaja na kuondoka bila ya
kushughurika na waya wala kuchomeka lakini
urahisi huu unawezesha teknolojia hii kuwa na
matumizi makubwa zaidi mfano barabarani
magari yanayotumia umeme yanaweza
kuchajiwa katika mataa ama katika sehemu za
maegesho.
Teknolojia hii kimsingi inachukua teknolojia
inayotumiwa na transforma ambapo kwenye
chaja yenyewe kuna kuwa na koili ambazo
pindi zinapo pitishiwa umeme hutengeneza
nguvu za usumaku ambazo hutumiwa na koili
zilizo katika kifaa chako kutengeneza umeme
tena ambao hutumika kuchaji betri ya simu
ama gari ama kifaa chochote husika.
Pamoja na kuwa ni rahisi kutumia teknolojia hii
ya kuchaji vifaa mbalimbali lakini pia
teknolojia hii inatumika zaidi kuchaji vifaa
vya baiolojia kama moyo wa bandia kwa
kuvichaji kwake ni njia salama mfano
haihusishi kuingiza waya ndani ya mwili, njia
hii pia inasemwa kwamba ni njia ambayo
inadumu muda murefu bila kuchakaa hii ni
kwasababu hakuna kuchomeka chomoa kama
njia nyingine (watumiaji wa chaja za simu za
iPhone watakubaliana na mimi jinsi chaja zetu
zinavyochakaa).
Picha kwa hisani ya mtandao ikionesha jinsi
teknolojia hii inavyofanya kazi
Chenye mazuri huwa hakikosi kasoro!
Teknolojia hii pamoja na mazuri yake ukweli
ni kwamba teknolojia hii inatumia muda mrefu
zaidi kuchaji kulinganisha na njia ya kawaida,
hii inasababisha watengenezaji wengi
washauri kwamba watumiaji wa chaja hizi
kuchaji kwa mara ya kwanza kwa njia ya
kawaida. Pia teknolojia hii ya kuchaji kwa
wireless inagharama kubwa kutengenezwa
ukiringanisha na chaja za kawaida.
Kama ilivyo kwa kila teknolojia inakuwa na
muungano wa wadau wa teknolojia husika
ambao unatengeneza viwango ambavyo ndio
huongoza utengenezaji wa vifaa
vinavyotumiwa na teknolojia hiyo basi
teknolojia hii ya chaja za wireless inatawaliwa
na miungano miwili mmoja ni ule wa Wireless
Power Consortium ambao unaungwa mkono na
watengenezaji wa simu kama Nexus LG
Microsoft na HTC na muungano mwingine ni
ule wa Power Matters Alliance ambao wao
wanaungwa mkono na kampuni la simu za
mkononi ya AT&T ya nchini Marekani
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon