Wakati Mbwana Samata akiwekewa vikwazo
kuondoka TP Mazembe, hali ni tofauti kwa
Thomas Ulimwengu, ambaye yeye mambo
yamemnyookea.
Mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe,
Thomas Ulimwengu ameshakamilisha
mazungumzo na Klabu ya Saint Etienne ya
Ufaransa na kinachosubiriwa ni yeye kusaini
mkataba wa kujiunga na klabu hiyo.
Ulimwengu amesema kabla ya dirisha dogo
la usajili barani Ulaya kufungwa mwezi ujao
tayari atakuwa ameshatua Ufaransa kuanza
maisha mapya ya kusakata kandanda barani
ulaya.
Ulimwengu ameileza StarTv kuwa mmiliki
wa TP Mazembe, Mose Katumbi amebariki
kuondoka kwake.
Ulimwengu ameweka bayana kuwa
amechagua kwenda Saint Etienne kwa kuwa
klabu hiyo inamsajili moja kwa moja bila
kufanya majaribio.
Klabu ya Saint Etienne inayoshiriki ligi kuu
nchini ufaransa kwa sasa inashika nafasi ya
5 katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa nyuma
ya point 4 na timu ya Monaco inayoshika
nafasi ya pili na point 34.
Hii ni kusema kwamba kama dili la
Ulimwengu litakamilika na Saint Etienne
ikamaliza nafasi ya tatu za juu basi Thomas
Ulimwengu atakua Mtanzania wa kwanza
kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya yaani UEFA CHAMPIONS
LEAGUE.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon