uchaguzi wa kuwachagua Mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala

Hatimaye baada ya danadana za muda mrefu,
uchaguzi wa kuwachagua Mameya wa Manispaa
za Kinondoni na Ilala, umefanyika na Umoja wa
Vyama vinavyunda Katiba ya Wananchi (Ukawa)
wamefanikiwa kuongoza Manispaa hizo.
Chaguzi hizo zilizhairishwa mara mbili kutokana
na mvutano uliotokewa katika chaguzi za nyuma,
ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kwa amri za
mahakama.
Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni, Diwani
wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface
Jacob amefanikiwa kuwa Meya wa manispaa
hiyo baada ya kushinda kwa kura 38 dhidi ya
mpinzani wake, Benjamin Sitta wa CCM aliyepata
kura 20. Naibu Meya ni Diwani wa Tandale kwa
tiketi ya CUF, Jumanne Ameir Mbunju.
Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala leo pia uliingia
katika mgogoro kati ya madiwani wa CCM na
wale wa Ukawa, hali iliyosababisha CCM kususia
uchaguzi huo na kuwaacha Ukawa kupiga kura
peke yao na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
kumtangaza Charles Kuyeko (Chadema) kuwa
mshindi wa kiti cha Meya wa Ilala kwa ushindi
wa kura 31, wakati Naibu Meya ni Omary
Kumbilyamoto (CUF) ambaye amepata kura 31.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post