Tamko Sahara Media Group kuhusu kufungiwa vyombo vyake.

Manejimenti ya sahara media group
ikizungumzia juu ya taarifa hizo imesema
haijapata barua au taarifa rasmi yeyote
kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania
TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake,
Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo
ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia
leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni miatano hadi
kufikia mwezi October 2015.
Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya
mara kwa mara kati ya TCRA akanda ya
Mwanza, makao makuu na sahara media
group limited nakukubaliana juu ya utaratibu
wa malipo ya ada husika.
lakini menejimenti imeshangazwa na hatua
hiyo ya TCRA kutanagaza kuvifungia vituo
vyake kupitia kutano wa vyombo vya habari
bila kujali athari zakufungia vyombo vya
kitaifa kwa walaji na watoa huduma.
Sahara media group limited imekuwa
ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za
kimarekani jambo ambalo limekuwa
likipandisha ada hizo kila mara na kufanya
ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama
kwama.
Menejimenti pia imelaani kwa taarifa hiyo
kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo
husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada
wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio
siku za kazi.
Menejimenti ya star tv inawaondoa
wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake,
hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza
tatizo hili kwa sahara media group limited
na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria,
Kanuni Na Maridhiano.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post