Baada ya kusimama kwa wiki moja ili kupisha mechi za Kombe la FA, Ligi KuuTanzania bara mzunguuko wa pili umeanza kwa vilabu vya Ligi Kuu kurudi uwanjani, uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, Simba walikuwa wenyeji waAfrican Sports wakati ambao watani zao wa jadi Yanga walikuwa Tangakucheza na Coastal Union.
Simba walikuwa uwanja wa Taifakurudiana na African Sports ambao mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga September 12 2015 waliwafunga kwa goli 1-0. January 30 2016 African Sports walirudi tena kuvaana na Simbakatika mchezo wa mzunguuko wa pili.
African Sports wameendeleza kuwa vibonde wa Simba baada ya kukubali kipigo cha goli 4-0, magoli ya Simbayalianza kufungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamis Kiizadakika ya 14, Hassan Kessy dakika ya 31 na dakika ya 43 Hamis Kiizaalifunga goli la tatu kwa Simba, kabla yaHaji Ugando hajapachika goli la nne dakika ya 75 kipindi cha pili.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa January 30
EmoticonEmoticon