Serikali yaitaka bodi ya dawa MSD kusafisha
wezi wa dawa mkoani Arusha.
Serikali imetoa siku 14 kwa mkurugenzi
mkuu wa bodi ya dawa kuhakikisha
watendaji wote wanaotajwa kuhusika na
mtandao wa wizi wa dawa na walioshindwa
kuchukua hatua wanawajibishwa kabla hatua
kubwa zaidi hazijachukuliwa.
Akizungumza wakati anazindua duka la MSD
kanda ya kaskazini lililopo katika hosipitali ya
mkoa wa Arusha ya Mount Meru naibu waziri
wa afya Dr. Hamisi Kigwangala amesema ni
jambo lililoko wazi na lisilo na shaka kuwa
ubadhirifu upo na wahusika wapo hivyo ni
bora yaliyoko ndani ya bodi yakafanyika
kwani hakuna njia ya mkato.
Aidha Dr Kigwangala amesema kimsingi MSD
inajitahidi kufikisha dawa kwa walaji lakini
jitihada hizo haziwezi kuwa na tija kama
baadhi ya watendaji wezi na wasiowajibika
wataendelea kupewa nafasi na amefafanua
na amewataka wasimamia dawa za serikali
wakati serikali ikiendelea kuhakikisha kuwa
dawa zinakuwa na nembo.
Akizungumza baada ya kufunguliwa kwa
duka hilo lililogharimu milioni 47 mkurugenzi
mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu,
amesema kazi ya kukabiliana na wizi wa
dawa, kuchukua hatua kwa wanaohusika
inaendelea sambamba na kufungua maduka
ya dawa kwenye mingine ukiwemo wa
Mbeya.
Duka hilo lililofunguliwa Arusha litakuwa
likihudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ya
Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
zenye vituo vya afya 919, zahanati 852.
Hospitali maalum, na hospitali za rufaa.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon