Athari Za Mvua Mwanza Jeshi la zima moto na uokoaji latupiwa lawama


Baadhi ya wakazi wa eneo la mabatini jijini
Mwanza wameendelea na zoezi la
kumtafuta mtoto Jesca… anayesadikiwa
kufa maji baada ya mvua kubwa kunyesha
jijini humo.
Licha ya kuendelea na zoezi la kumtafuta
mtoto huyo kwa kutumia dhana duni wakazi
hao wamelitupia lawama jeshi la zima moto
na uokoaji kwa kutoshiriki kikamirifu katika
uokoaji wa watu waliozama maji.
Wanasema jeshi hili ndilo lililo na ujuzi na
vifaa vya uokoaji tofauti na matumizi ya njia
za asili ambazo hazina uhakika.
Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi
kaimu kamanda wa jeshi la zima moto na
uokoaji mkoa wa Mwanza kamishina
msaidizi Hamidu Nguya amesema jeshi hilo
mbali na kuwa na jukumu la kuzuia majanga
jamii inapaswa kufuata maelekezo ya
wataalam wa jeshi hilo ili kukabiliana na
maafa au kutoongeza ukubwa wa tatizo.
Mama mzazi wa marehemu akiwa eneo la
kliniki darajani pamoja na watu waliokuwa
wanaendesha zoezi la utafutaji mwili wa
mwanaye amesema alipata mshituko
kutokana taarifa ya mwanae kuzombwa na
maji.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza
Justus Kamugisha amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post